SHUJAA WA AFRICA BLOG

Wednesday, August 15, 2018

NDEGE YA RAISI Ep1


NDEGE YA RAISI:
NA MUSTAPHA J. KIROBOTO                                                                            (RIWAYA)
Mlio mmoja wa siraha ya kitecnolojia ulinipelekea usingizi kukatika ghafla na kukurupuka kutoka kitandani, Haikuwa ndoto bali ni uhalisia na nyumba iliyokuwa imevamiwa ni ile ninayoishi, nililala bila kuzima taa kutokana na uchovu hasa kutokana na mazoezi yetu sisi makomandoo wanchi hii, bila ya shaka watakuwa ni wazee wa kazi, nikakurupuka kwa kasi sana kuliendea kabati ili nitoe bastora yangu, manake sikulala nayo kitandani siku ile kwakua usingizi ulinipitia tu, kabda ya kulifikia kabati umeme ukakatika na ghafla nikasikia kitu kinaburuzwa kwa,kasi pale ndani kiasi kuniogopesha na kunifanya nirudi nyuma, ndani ya sekunde tano tu umeme ukarejea cha kushangaza kabati pale mbele nikaliona limehamishwa umbali mkubwa tu kutokana na ukubwa wa chumba changu, ninani ameweza kulisogeza kabati kubwa namna hii ndani ya sekunde? Kabda sijapata jibu, "karibu katika mlango wa kifo" sauti nzito ilipenya masikioni mwangu kutokea nyuma yangu, nikageuka kwa kasi sana nikakutana na kibonge cha mtu, ni mkubwa na mpana sijapata kuona, kwa haraka nikahisi kuwa ni mtu wa miujiza, "wewe ndie uliesogeza kabati langu?" Nilijipa ujasili na kumuuliza, Hata ukijua haitakuwa na manufaa kwa sasa, weka mikono kichwani na upige magoti, picha ya mtu kama huyu niliwahi kumuona nayo Alicia nouthon, mke wangu niliemuoa kwa mkataba kule Detroit , Michigan America nilipokuwa nimeagizwa na serikali kuchunguza vyanzo vilivyohusika kuingiza siraha kinyemela hapa nchini nikashangaa na kumhoji akaniambia ni picha ya ubunifu hakuna mtu kama huyu duniani, sasa mbona leo hii yupo mbele ya macho yangu!? Ni kweli ndie yeye hata sura ndie huyu. Samahani sana brother... nahisi kuna sehemu nilishawahi kukuona? Laiti ungejua unaongea na nani usingethubutu kuhoji hata swali moja... pumbaavu kaachini, lakinii mtu mkubwa kama huyu amepitaje katika mlango wa chumba changu, kwa haraka haraka akili iliniambia nitazame mlangoni::       
 Ndio mkuu hatuna taarifa za kuingia kwa ndege hizo za kitecnolojia katika nchi yetu lakini ni ukweli kuwa ndege hizo zimevamia nchi na sasa zipo maeneo ya ostabay, upesi sana ongea na makao makuu ya jeshi la anga wadhibitiwe, je Unavyoona ni ndege za nchi gani zilizovamia nchini usiku huu? Zina alama ya bendela ya America, ila kinaonekana ni kikosi maalum cha uchunguzi, upesi taarifa zifikishwe ikulu na makao makuu, Ilikuwa ni makao makuu ya usalama wa nchi,::
 bila ya shaka hawa jamaa walioingia ni kikosi maalum lakini kwanini wafikie kwangu,::
 upesi mtorosheni mheshimiwa raisi muwekeni eneo salama, mkuu wa usalama wa raisi aliongea huku akitelemka ngazi mbio mbio hadi chumba maalum cha usalama, vipi antony, aliuliza kwa hofu, Hakuna mawasiliano yoyote yanayotoka ama kuingia, kila kitu kimezuiliwa, antony alijibu huku akihama computer contral room moja hadi nyingine, "wazuie wasitumie ndege kumuondoa mheshimiwa Raisi hakuna mawasiliano ya aina yoyote" Catheline mwanadada mrembo wa control room namba mbili alimtahadharisha Antony alie ingi eneo lake huku akinyanyuka kutoka eneo aliloketi upesi na kuwahi upande wa emegency kujaribu kuiuliza computer ili kujua tatizo, Mungu wangu tutawapata vipi makao makuu ya mawasiliano, Antony aliongea huku akiwahi eneo lenye Radio call, Punde mr mzirai akaingia eneo lile kwa kuchanganyikiwa "si Radio call wala simu za kawaida kwangu vyote havina mawasiliano" aliongea mr mzirai huku akiingia kauli iliyozidi kumchanganya Antony. Inamaana hata radio call hazina mawasiliano? Antony aliuliza huku akihakikisha, niliingia kwenye ofisi yako sikukukuta antony vipi nawewe uko huku, tatizo ni la wote mzee wangu, vipi cathelin umeambua nini? Mkongo wa taifa wa mawasiliano umezimwa na mitambo maalum ya kisasa na kuzuia kila aina ya mawasiliano, Niliongea wazuie wasitumie ndege kumuondoa mheshimiwa, Antony alitoka mbio mbio kuwahi kwenye maegesho ya dharula ili kuwazuia wakuu wa usalama wa Raisi wasitumie ndege,::
 Unadhani ni kitu gani kimetokea kwenye nchi yangu? Mheshimiwa Raisi aliuliza huku akifunga mkanda baada ya kuketi kwenye Siti ndani ya ndege yake, ndege za kisasa zenye teknolojia ya hali ya juu zimeingia nchini bila taarifa yoyote na hatuelewi ni kwa nia gani, alijibiwa, Zimetokea nchi gani, Hatuna uhakika ila zina alama ya bendera ya America, kama ni mmarekani ni lazima nitampiga, nitamtumia ndege za kivita zimshambulie huko huko na niiteketeze New york. Namuda huo tayari ndege ilishaanza kuvuta kasi na hatimae kupaa, ndege no Af, 58C JET iliyobeba familia ya Raisi inagoma kuwaka, rubani wa ndege ya pili aliongea bila kupata mawasiliano, Jamani, mbona mawasiliano hakunaa,, na ndege ya mheshimiwa imesha enda angani,
antoniiiii... catheline aliita huku akiwahi mbio mbio... antony anageuka huku akiendelea kutembea kinyume nyume, izuie ndege ya familia ya raisi isipaee namuona muheshimiwa ameshapaa,,,, catheline alimpazia sauti antony... ongea na kikosi maalum chukueni helcopter mumuwahi mheshimiwa....
 Pengine ni ndege ina matatizo unadhani Gerald angethubutu kuidiriki anga kama mawasiliano yange kuwa hakuna hali amem beba mheshimiwa?, Marick rubani msaidizi aliongea huku akijaribu kuiwasha ile ndege, ndege ikawaka, tuiondoshe familia ya mheshimiwa haraka....
Mueleze mheshimiwa kuwa ndege yetu haina mawasiliano yoyote... vipi nijaribu kutua? Gerald Rubani wa ndege aliyokuwemo Raisi alimueleza mkuu wa usalama wakiwa angani, punde ndege kubwa ya Green planet international iliyokuwa inatokea South korea kuja Dar es salaam Tz iliwakosa sehemu ndogo sana na kuangukia baharini, Kitu gani kinatokea? Mheshimiwa Raisi alihoji kwa hofu, ndege ya Green planet international imetukosa na kuangukia baharini... "mkuu ndege haini sapoti nikiiongoza inaenda itakako,,, Gerald aliongea kwa kuchanganyikiwa bila ya kujua afanyenini na wakati huo ndege ikajiongeza spidi yenyewe... Ndege yeyote iliyoko kwenye anga la nchi yetu haiwezi kuongozwa bali hujiongoza yenyewe... hatuwezi kurusha helcopter ni sawa na sifuri, Aneth Rubani mkuu wa helcopter za ikulu aliongea huku akijaribu kuiamsha helcopter hivyo hivyo... na muda huo ndege iliyobeba familia ya Raisi ilipita kasi karibu na pale na kushika anga,"Antony anafanya ninii..."catheline aliongea kwa kuchanganyikiwa...Aneth paisha helcopter hivyo hivyo tukawasaidie.....Itaendelea...

Usisahau ku Follow Page hii ili kujihakikishia kuipata Riwaya hii Kila inapotumwa pamoja na Riwaya ijayo ya Safari ya kuzimu
+Mtunzi+ Mustapha J Kiroboto. (Moost Jay)

Facebook         Mustapha J Kiroboto.
Whtssp            +255 784 944 804
Youtube:          Shujaa wa Africa Tv

Tukutane sehemu ya pili

No comments:

Post a Comment