SHUJAA WA AFRICA BLOG
Tuesday, May 18, 2021
Monday, May 3, 2021
NDEGE YA RAISI
(Riwaya)
EP 3
Ilipoishia... punde mitambo maalum yakisasa ya kudhibiti siraha za kiatomi ikawashwa na ile ndege ya kitecnolojia ikaanza kuamka kwenda angani kitu kilichopelekea kile kipande cha mtu kunikalisha chini na punde upepo mkali wenye baridi ya unyevu kushinda AC ya kawaida ukaanza kutawala pale ndani... nikagundua sababu ya wenzangu wote kuvaa ma jacket ya baridi.... Endelea....
Upesi sana profesa Shivji aligeuza kiti chake na kuanza kucheza na mitambo ili kupambana na waliokuwako nje, kupitia screen maalum nikaweza kuona ndege hizo zenye nembo ya Tanzania, bila ya shaka wenzangu wamekuja kuniokoa.. Wamepata wapi mawasiliano hawa watu Richard.... prof shivji aliuliza kwa kuchanganyikiwa huku akiendelea kuzungurusha mitambo maalum ya kisasa ili kujihami,.. hupaswi kuuliza kwasasa chamsingi ni kuwadhibiti ili tuweze kuondoka kwenye hiki kinchi... mtu wenu si mumeshampata? Mwantumu alijibu huku akiendelea kutafuta shabaha kwenye vifaa maalum vya kiusalama:: Yeaaah... Tumefanikiwa... sasa angalia namna ya kuwadhibiti mbwa hawa..... Safi sana meja.... zitafute ndege zetu ishirini na nne zilizojitoa mhanga kuelekea ostabay bila ya mawasiliano.... yalikuwa ni makao makuu ya ulinzi na usalama wa Taifa... viongozi wa kitengo hicho walionyesha furaha baada ya kufanikiwa kurejesha mawasiliano kutumia mitambo ya dharula iliyotengenezwa na wataalam wa jeshi la marekani miaka michache nyuma, mitambo hii imeunganishwa moja kwa moja na comunication control unit inayo ongoza ikulu ya america kimawasiliano. Na huu ndio mkataba mkuu wa maraisi wa Tanzania na America hata Tanzania kumpatia mmarekani ardhi ya kigamboni, ni ngumu kuizima mitambo hii maana utazima mpaka mawasiliano ya ikulu ya marekani (white house)... Qahell - 313 yaseen T54D... nakupata mkuu... nipo ostabay eneo la tukio... ni eneo yalipo makazi ya Daniel manana komando mwaminika wa Tanzania.... mmoja wa marubani wa Qahell - 313 mwenye pass namba T54D alipata mawasiliano na makao makuu ya ulinzi na usalama wa nchi, "Hebu nipe matumaini T54D.... mkuu inavyoonekana ni njama ya Daniel manana comando wa Tanzania::
Sasa inakuwaje aneth... sielewi catheline... matokeo ni mwisho wa uwepo wa eneo wazi naamini helcopter yetu itagonga nakulipuka.... ilikuwa ni ndani ya helcopter waliyokuwemo catheline na Aneth.... upesi catheline alihamia nyuma nakufungua kibox maalum ila hakuona alichokihitaji... Parachut ziko wapi Aneth?... kumbuka helcopter hii ilitumika kwenye maonyesho ya miaka mia moja ya jeshi la ulinzi... nadhani parachut hazikurejeshwa.... mara vifaa vya mawasiliano vikawaka pale ndani... "kitu gani aneth?".. mawasiliano yamerejea.... je ndege unaweza kuiongoza tena... hapana... bado inajiongoza yenyewe mkuu wangu... upesi catheline akawahi eneo lambele na kuvaa kifaa cha mawasiliano... Afisa usalama T892F kitengo maalum ikulu.. catheline jastine mhenga... makao makuu ya usalama nakusoma 892F... Taarifa rasmi tukio la uvamizi wa ndege za kitecnoloji.... wakuu wa usalama wa Raisi wamemuondoa mheshimiwa ila muda mwingi hapakuwa na mawasiliano angani.... nakusoma 892F... ni muda gani umepita tangu tukio hilo litokee... Takribani dakika Arobaini na tano hivi... na mbaya zaidi ndege zikifika angani hugoma kuongozwa na rubani.... ok... subiriii... Robert haule mkuu kitengo nyeti usalama wa nchi aliacha kuongea na catheline na kukimbilia chumba maalum.... mheshimiwa Raisi yupo angani Donald... upesi tafuta mawasiliano na Grlard rubani wa ndege yake.. aliongea haraka haraka huku akiingia chumba kile... ni muda gani yuko hewani Donald alihoji huku akiitafuta ndege ya Raisi Angani.... yasemekana kama dakika 45 zilizopita... AF 59C jet.... unanipata.... (kimya)... Af 59C jet.... unanipataa...(kimya) Mkuu...mheshimiwa alitumia ndege gani kwenda angani... Donald aliuliza huku akiwekawazi mawasiliano yote ya anga, upesi muulize Catheline... nimekosa mawasiliano nae muda mrefu tu ofisini, mcheki angani nilimpata angani... ndege gani mkuu... ni helcopter ya mashambulizi... T892F... "T892F... 64D... makaomakuu unanipata?.... wakati huo ndege ya kina catheline ilijiongeza spidi kwa kiasi cha kuogopesha... catheline alichukua Reseiver bila balansi maalum huku upepo mkali ukimpiga usoni kiasi nywele zake kufumuka kwa kupeperuka... Donald naku pata Donald nakupataa...catheline alijibu kwa sauti ya juu kuupinga upepo... vizuri T892F... Tafadhari nijuze mheshimiwa ametumia ndege gani kuelekea angani.... catheline kabda hajajibu helcopter iliyumbishwa kwa kasi sana... kitu kilichopelekea catheline kuchomoka toka kwenyekiti na kuning'inia kuelekea nje akishikiliwa sehemu ndogo na mkanda... Aneth nisaidie tafadhariiii... alipiga kelele huku akijitahidi kutafuta eneo la kushika...Upesi aneth alijivuta ili amshike catheline ghafla mfuniko mzito wa box alilolifungua catheline awali ili kutafuta parachut ukampiga Aneth na kisha kuujeruhi mkanda uliomshika Catheline na wenyewe kuanguka kwenda chini, Aneth akapoteza fahamu huku mkanda uliomshika Cathelin ukiendelea kukatika taratibu kwa kila helcopter (hawk) ilivyokuwa ikiyumba... Aneeeeth.... catheline aliita kwa sauti ya juu huku akiuangalia mkanda unavyozidi kukatika... Halo T 892F... sikupati tafadhari... Donald aliendelea kuita bila mafanikio... na muda huo Helcopter ikageuzwa kwa kasi kiasi catheline akawa anatarajia kuanguka kuliendea feni la ile helcopter lililotengenezwa kwa madini magumu ya steel hadner...huku mkanda ukizidi kukatika... Aneeeeeth... aliita bila mafanikio muda huo Aneth akiwa amezuiliwa na mkanda pia huku chupa za asidi zilizo kwenye lile box zikiminywa na kukaribia kupasuka ili acid ile hatari inayosafishia siraha kumuelekea Aneth, Rubani mwaminika na sniper mahiri aliehitimu mafunzo yake kwenye chuo cha West Point - The U.S. Military Academy kilichopo america... alipata kuaminiwa sana na serikali baada ya kuweza kuushinda mtihani wake wa mwisho vizuri na kupata alama za juu... Aneth ni mtoto wa pekee kwa mama yake bi Grolia mathew ambae kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa figo nae aneth ndie msaada kwa mama huyo... kifamilia hakuolewa ila alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike (Natasha Anderson) aliemzaa na Mr hallk anderson mmarekani mvuvi aliefariki baada ya boti yake ya uvuvi kupotea na baadae kuthibitika kuzama baharini karibu na Visiwa vya Virgin vya Marekani (United States Virgin Islands) baba huyu alifariki pindi Aneth akiwa na ujauzito wa siku tisa. Natasha Anderson anasoma kwenye shule ya Sandy Hook iliyoko katika jimbo la Connecticut kaskazini mashariki mwa Marekani. shule hiyo ya msingi iliyopo mji mdogo wa Newtown, umbali wa kilomita 90 kutoka New York.. kutokana na Natasha kutamani sana kuwa na baba kama watoto wenzake mara nyingi Aneth alimuambia ajivunie kuwa na mama kwani wapo waliomkosa na pia kumuimbia wimbo unaosema "mimi ndie mama yako nami ndie baba kwako.. chochote utakacho sema we mtoto mzuri mtoto wee ntakuongoza vema mtoto mzuri mtoto we... nitakukuza nasema mtoto mzuri mtoto we... nakusimaia maisha yakooo.... muda huo injini ya helcopter ilianza kuzunguruka kwa misi kwakua helcopter iliinama kwa muda mrefu kiasi mafuta kushindwa kutumika vizuri bila ya shaka ilielekea kuzima::
Ni saa sita za usiku sasa madam aliendelea kum bembeleza Natasha ili alale kwani ni zaidi ya masaa mawili alikuwa kwenye simu ya mezani akimpigia mama yake kipenzi (Aneth) simu ambayo iliita tu bila majibu yeyote... ni kawaida ya Natasha kuongea na mama yake kabda ya kulala na leo ni mara ya kwanza kwake kutopokea simu ya binti yake huyo wa pekee kitu kinachozidi kumkosesha furaha Natasha alie ng'ang'ania simu huku machozi yakimtoka... Natasha tafadhari naomba ulale.... kesho asubuhi nitampigia tena mama yako naamini atapatikana na utaongea nae... usimwage machozi yako tafadhari... pengine mama yako amechoka kupitiliza usiku wa leo.... madam wa bweni alilopo natasha aliendelea kumsihi Natasha na kuendelea kuwa pamoja nae... madam...nampenda sana mama yangu... nimzazi wangu pekee tambua hilo... nina hofuu... si kawaida yake kulala bila kuniimbia... Natasha aliongea kwa kulalamika::
Kitu gani kinatokea.. mbona ndege inaenda hovyooo... mr andrew makema alihoji akiwa kwenye ile ndege kubwa sana iliyobeba familia ya raisi... mkuu funga mkanda bara bara usiamke kitini naamini sasa ndege yetu imefikia tatizo kubwa sana na sasa inaanguka... marick alijibu huku aking'ang'ania kiti bila kukaa lengo lake ni kuifikia power unit ambayo imegoma kuzalisha umeme baada ya generetor la ndege hiyo kuzimika ghafla,Ndege inaanguka... Andrew makema aliuliza kwa mshtuko mkubwa na kumshtua sana Paull Rafael makema mtoto wa kwanza wa Raisi na katibu mkuu wa chama cha Raisi huyo ambapo pia ni mwanafunzi wa shahada ya uongozi pale mlimani... nani kasema ndege inaanguka... aliuliza kwakuchanganyikiwa.... mtu yeyote asitoke kwenye kiti chake tafadhari... tunajitahidi kupambana na tatizo hili tunawaomba mfunge mikanda yenu vizuri... marick aliwatahadharisha, paul Rafael makema ana uhusiano wa kisiri na catheline mwana usalama kitengo maalum ikulu, paul amempenda sana catheline ila tatizo catheline anapenda sana maisha ya kujirusha... hufanya hivyo kwa siri kila anapopata rikizo... anaefahamu mahusiano ya cathelin na paull ni mwanadada Aneth (Rubani mkuu wa helcopter za ulinzi wa ikulu na sniper mwaminika) na hasa ni kutokana na urafiki wa aneth na catheline... catheline na Aneth walionana kwa mara ya kwanza 1232 22nd St. NW, Washington D.C 20037 kwenye ubarozi wa Tanzania nchini america ambapo walifahamiana ila hawakutaraji kuwa wangefanya kazi pamoja. Harufu ya shoti ya umeme ilianza kusikika ndani ya ile ndege iliyoibeba familia ya Raisi kitu kilichozidi kumchanganya Rubani... Marick... jitahidiii zima kabisa upande wa jenereta tegemezii.... Rubani alimpazia sauti marick ambae tayari alisha ingia chumba cha mitambo ya ndege hiyo ambayo ilishaanza kushika kasi kuelekea chini... marick huku akigeuzwa kila upande kutokana na ndege ilivyokuwa ikijigeuza geuza angani aliifikia power unit ya ndege hiyo na kugundua kuchomoka kwa moja ya teminal inayotoa umeme kwenda kwenye matumizi ya ndege hiyo... kwatabu sana aliichomeka ile teminal na punde umeme ukarejea kwenye ndege yote na taa kuwaka... Asante marick...asanteee... Rubani aliongea huku akijivuta na kuwasha injini za ndege ile kubwa.. injini zote sita zikawaka na rubani kujitahidi kuiweka sawa ile ndege punde ndege ika kaa kwenye muelekeo mzuri kiasi watu wote waliokuwemo kwenye ile ndege kushangilia kwa furaha..Bado sijaruhusu mtu kunyanyuka kutoka kwenye kiti chake tafadhari mikanda isifunguliwe kwa yeyote... Rubani alitahadharisha ... marick alirejea chumba cha kuongozea ndege haraka haraka akiwa na furaha ya kutoamini... Tumefanikiwa . Aliongea kwa furaha... "ila kuna kitu sikielewi" rubani wa ndege ile alitahadharisha... kitu gani tena... mara ving'ora vya hatari vikaanza kulia ndani ya ndege... vipii kitu gani? Marick alihoji kwa hofu."mungu wangu... injini namba mbili inawaka moto... Rubani aliongea kwa kuchanganyikiwa... kitu gani tufanye... upesi sana ndege iteremke chini.... sawa jitahidi kama tutawahi... Ving'ora vyanini jamani mbona ni hatari sasa... mkuu injini namba mbili imepata hitirafu ya moto... Telemsha ndege chini, Andrew makema aliamrisha, na muda huo ndege ikajiongeza mwendo na kutoka kwenye muongozo wa rubani... mungu wangu ndege haiongozeki nitakavyo mimi inakwenda yenyewe... Rubani aliongea kwa kuchanganyikiwa huku injini ile namba mbili iliyokuwa upande wa kulia mwandege ikizidi kushika moto kiasi ndege ile kuonekana mfano wa kimondo chenye kasi kubwa angani... nilikwambia uzime jenereta sidhani kama ulizima marick... punde ndege aina ya Airbus A380-800 ambayo ni ndege kubwa ya kwanza ya kubeba abiria duniani ya shirika la ndege la ujerumani Air Lufthansa ilionekana kuja kwa kasi ya ajabu ni wazi kuwa nayo ilipoteza muelekeo... kuna hatari ya ndege hizi mbili kukutana uso kwa uso.. napengine hii ndio itakuwa ajari kubwa na ya kwanza kwa ndege hizi mbili zenye sifa kubwa Duniani yaani ndege hii kubwa ya kwanza duniani inayobeba abiria na mizigo inayoitwa HAV304. Iliyotengenezwa na kampuni ya Hybrid Air Vehicles kiufupi ndege hii iliyobeba familia ya Mheshimiwa raisi Inauwezo wa kukaa angani kwa muda wa wiki 3 na nusu mfurilizo pia na sehemu ya kubeba abiria 50 pamoja na tani 50 (kilogramu 50,000) za mzigo mengine. Ki uwezo inauwezo wa kutua kwenye barafu, Kutua kwenye maji na nchi kavu. Ina sehemu ya paking za helicopter na pia paking ya ndege ya abiria ya kawaida, hivyo ndege hii haihitaji uwanja ili kutua.... ni ndege inayotazamwa na dunia kwa ubora wake ila hii ilikuwa ni oda maalum ya ikulu ya Tanzania hivyo iliongezwa vifaa zaidi vya kujilinda... pia ndege hii ya Airbus A380-800 inafahamika kuwa ni ndege kubwa ya kwanza duniani ya kubeba abiria.... osalalaaa... ajarii... captain silovich mac teener Rubani mkuu wa Air Rufthansa aliongea kwa kuchanganyikiwa.. ni ndege kubwa sana iliyo mbele yetu pengine huu ukawa mwisho wa maisha yetu bora kile kidege cha kifahari tulichokigonga awali... aliongeza mc teener.... mungu wangu anga ya Tanzania inanini... alihoji msaidizi wake huku akijaribu kuiongoza ndege hiyo kubwa bila mafanikio:: Kumetokea nini kwenye ndege yetu... mheshimiwa Raisi alihoji huku jasho jingi likimtoka licha ya Ac kuendelea kuzalisha hewa ya baridi mle ndani ya ndege ya Raisi.. eti Gerald nini ndege yetu imegonga muda mfupi... afisa usalama wa karibu na raisi alimpazia sauti rubani wa ndege hiyo.... Ndege kubwa ya Airbus A380~800 ya shirika la ndege la ujerumani Air Lufthansa imegonga eneo lachini la ndege yetu... ndege yetu imesalimika...alihoji mheshimiwa... Naendelea kuchunguza mheshimiwa.... Gerald akafanikiwa kuiongoza ndege na kuimiliki vizuri ila bado ndege hiyo ilikuwa nje na mawasiliano ya waongoza ndege wa ardhini (watu wa rada), haikuonekana kwenye rada wala kifaa chochote cha mawasiliano... vizuri sana naona ndege imetulia ninaweza kuiongoza sasa.... Gerald aliongea kwa furaha huku akiweka vizuri mitambo yake, nieneo gani tupo... afisa wa mambo ya dharula yanayotokea ikulu aliingia chumba cha rubani na kuuliza...sijafahamu ni wapi tupo japo yazaki inaniambia tumetembea zaidi ya kilometa elfu moja mia moja kwenda angani na kilometa mianane ishirini na sita kwenda mbele kuanzia tulipotoka ikulu magogoni Dar es salaam na bado ndege yangu haina mawasiliano yoyote... mara alama ya tahadhari ikawaka.... mkuu inavyoonekana ndege ya Air Lufthansa iliyotugonga imetoboa tenk la mafuta ya ndege yetu... mafuta yanamwagika kwa wingi sana... +MTUNZI+ Mustapha j kiroboto (Moost Jay)
Subscribe to:
Posts (Atom)