SHUJAA WA AFRICA BLOG

Friday, June 16, 2023

NANI KURITHI MIKOBA YA NABI YANGA?

Ni swala la muda tu. hii ndio kauli inayotumiwa sana na mashabiki wa Young Africans sc japo ukweli kuondoka kwa kocha nabi kumeumiza vichwa vya mashabiki wengi wa yanga almaaarufu kama wananchi. lakini swali nikuwa, nani atakuwa mrithi sahihi wa kocha nabi? tetesi ni nyingi wapo wanaosema kuwa jangwani kunanukia makocha wakubwa wenye renk nzuri za kimataifa kama vile ibenge au mosimane. hakuna linaloshindikana lakini nini kipo kwenye vichwa vya viongozi wakuu wa yanga? kitu ambacho wana yanga wanatakiwa kujivunia ni uwepo wa mhandisi ersi saidi pamoja na uongozi wake kwani kabla ya hapo yanga hawakuwa na nabi wala mayele na bangala lakini scouting ya hersi ndio iliwaleta wamba hao kwenye club hivyo wasiwe na wasi kwani yule aliemleta nabi bado yupo na ana bafasi ya kufanya maajabu mengine japo nalazimika kuongea jambo moja tu kuwa, kwa mafanikio makubwa ambayo yanga wameyafikia ndani ya misimu miwili ila hasa msimu ulioisha, inahitaji umakini sana ili kufanya jambo sahihi