SHUJAA WA AFRICA BLOG

Sunday, August 13, 2023

Ngao ya jamii 2023.

Hatimae timu ya azam.fc imefanikiwa kuifunga timu ya singida big stars 

Mabao 2 - 0 kwenye mchezo wa ngao ya jamii wa kutafuta mshindi wa tatu. Kwa matokeo hayo timu ya azam fc imefanikiwa kukamata nafasi ya tatu huku singida big stars wakikubali kushika mkia.

Wakati huo mchezo wa fainali ya ngao ya jamii utachezwa leo ifikapo saa moja kamili za usiku (aug 13/2023) #Ligi_kuu_tanzania_bara

Thursday, August 10, 2023

YANGA YAICHAPA AZAM 2- 0 MKWAKWANI #NGAO YA JAMII 2023


 

Yanga 2 - 0 Azam

Maabingwa watetezi Yanga Sc wameendeleza ubabe kwa kuichapa azam fc mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali ya ngao ya jamii iliyofanyika uwanja wa CCM Mkwakwani katika jiji la Tanga. Magoli ya yanga yalifungwa  na Stephene azizi ki dakika ya 85 na bao la pili likiwekwa kambani na Clement mzize dakika ya 89

Kwa ushindi huo yanga inasubiri kukutana na mshindi kati ya simba sc ama singida FG utakaopigwa kesho tarehe 9 aug 2023