NDEGE YA RAISI:
NA MUSTAPHA J. KIROBOTO
(RIWAYA)
Sehemu ya pili
Ilipoishia.... muda
huo ndege iliyobeba familia ya Raisi ilipita kasi karibu na pale na kushika
anga,"Antony anafanya ninii..."catheline aliongea kwa
kuchanganyikiwa...Aneth paisha helcopter hivyo hivyo tukawasaidie.
Endelea......
Ni wazi kuwa
hatutafanikiwa catheline.... ni ngumu kuiongoza ndege ikisha shika anga tusije
kusababisha ajari kwa ndege zote tatu huko angani, Aneth alijibu huku
akiirejesha helcopta chini, Aneth nimekwambia paisha helcopter...una mpango
gani na maisha ya mheshimiwa?? Catheline aliongea kwa ukali... ila tatizo la
anga na mawasiliano nimekujulisha... Amri...paisha helcopter nauifuate ndege ya
mheshimiwa upesi nimuhamishe, Aneth akaamsha helcopter na kuidiriki anga...
vipi aneth Ndege ya muheshimiwa imeelekea huku mbona unakwenda hukoo?! Si mimi
ninaeipeleka catheline haitaki kwenda nitakako mimi:: Kitu gani tunatakiwa
kufanya kwa wakati,huu? Mkuu wa usalama wa raisi alimuuliza Gerald rubani wa
ndege ya raisi huku akizidi kuchanganyikiwa, sielewi ni spidi,kali mno
tunayopelekwa nakili tangu nianze kuongoza ndege sijawahi tumia spidi hii,
mungu wangu, vipi hali ya anga? Rada hazisomi... sina mawasiliano ya namna
yeyote... mlango wa chumba cha dharula unagoma kufunguka tafadhari vunja vioo
vya chumba toa parachut umpatie mheshimiwa, upesi sana mkuu wa usalama aliwahi
alikoelekezwa na rubani ili kuhakikisha Raisi anaendelea kuwa salama, Vipi juu
ya mwendo tunaokwenda kuna usalama kweli? Mheshimiwa Raisi alihoji huku
akijiweka vizuri kwenye kiti, muda mwingi natafuta mawasiliano na Rubani lakini
simptati...upesi nenda kaulize kama kuna tatizo tujue... Sawa mheshimiwa::
Tafadhari tujitahidi kuiongoza ndege irudi chini sielewi Dash board
inachoniambia... Rubani wa ndege iliyobeba familia ya Raisi aliongea kwa
kuchanganyikiwa... kuna niniii mbona ndege inakwenda tofauti.... kama kuna
hitirafu tujue... mr andrew makema ndugu wa karibu wa Mheshimiwa Raisi msomi
aliepewa cheo cha afisa usalama wa ikulu aliuliza, Ndege yetu haina mawasiliano
mkuu... upesi telemsha ndege chini... aliamlisha... Tafadhari mkuu ameamlisha
ndege ishuke chini... Taarifa ilifikishwa kwa Rubani wa ndege hiyo na muda huo
ndege ikageuzwa kwaajili ya kushuka chini ikiwa kwenye kona kubwa ya dharula
ndege ikapoteza mawasiliano na Muongoza ndege... punde taa zote za kwenye ndege
zikazimika... jamani kitu gani kinaendeleo huko mbelee.... naamini ni hitirafu
kubwa sana imetokea kwenye ndege yetu kwani inanigomea kuiongoza... Rubani
alijibu huku jasho likimtoka... Tufanye nini marick?... upesi cheki power unit
kama itaweza kuzalisha umeme .... Rubani alijibu huku akijaribu kuhangaika ili
kuokoa tatizo hilo.... punde injini za ndege hiyo zikazima kwa awamu na ndege
kuanza kurudi chini:::
Nikauona mlango wa chumba changu umeongezwa
upana kwa kukatwa ukuta kitaalam bila hata kuweka michanga, tii amri yangu kaa
chini, kile kipande cha mtu kiliniamrisha tena... nikamtazama kwa umakini na
kugundua kuwa hata ningempiga pigo kali kiasi gani lisinge mdhuru kutokana na
ukubwa wa mwili wake kwakuwa watu wa namna hii hata siraha za kuwadhuru huwa ni
maalum... taratibu nikapiga magoti mikono kichwani... punde akaingia mr allen
mcLeod, afisa usalama wa america alienipokea pindi nilipotembelea nchini mwao
kikazi, vipi ni ujio wa amani kwangu ama... bila ya kujibiwa swali langu
nikapigwa pingu na kutolewa hadi kwenye ndege za kisasa zenye tecnolojia ya
hali ya juu Zilizokuwa zimepaki nje ya nyumba yangu.. sifa ya ndege hizi niliwahi
kuipata nilipokuwa Saratov Rashia ni ndege zenye uwezo wa juu sana ki ulinzi,
na zaidi zina vifaa maalum vyakuweza kuzima mitambo ya mawasiliano kwa upana
wowote wa eneo unalotaka kulivamia, ndani ya chumba maalum kwenye ndege ile
nikawakuta mwanadada mwantumu hamisi kiondo akiendelea kuongoza mitambo, macho
yalinitoka nikiwa siamini ninachokiona::
Takribani miezi
tisa iliyopita Dunia iliwahi kupatwa hofu kubwa ya kuteketea kutokana na wana
sayansi wa kimarekani kugundua kuisha kwa mhimili mkuu ulioishika moja ya
asteoridi (Gimba kubwa au Jiwe lililo mfano wa sayari nyengine) ambapo ulibakia
nyuzi chache mhimili huu kukatika na tukio hilo kupelekea asteoridi hiyo ya
ukubwa wa kuizidi Dunia kwa zaidi ya takribani kilometa tilioni mia saba kila
upande ( mraba) kuiangukia Dunia na pengine huo ndio ungekuwa mwisho wa dunia
kwani kwa vipimo vya wataalam ilionekana Dunia ingeathirika kwa zaidi ya
asilimia mia moja na ishirini na nne ya eneo lake, Nchi nyingi kubwa Duniani
zilituma wataalam wake ili kupambana na tatizo hilo kwa ajili ya kuiokoa Dunia
lakini hali ilikuwa tete na mhimili huo ulioishika esteorid ulizidi kuathilika
kiasi cha kubakisha masaa mia moja stini na nne (164) sawa na siku saba (7)
kabda ya kukatika na kuiachia esteorid hiyo iliyokuwa imeelekea kuiangukia
sayari ya earth. (Dunia) Jopo la wanasayansi lililokuwa juu angani lilianza
kugawanyika kwa hofu, wengi walirejea ili kufa pamoja na familia zao ila
wengine walijitahidi kukaza madini ya namna mbali mbali kwenye mhimili huo
lakini kiukweli hayakuweza kuleta mafanikio, Wanasayansi wa Urusi walirudi
nchini kwao kwa dharula nakukutana na waziri mwenye dhamana ya mambo hayo...
urusi ilipata jina kubwa sana mwaka mmoja nyuma baada ya wahitimu wa sayansi ya
anga kufanikiwa kutengeneza kifaa maalum cha kuikinga Dunia na milipuko mikali
ya volcano iliyotokea huko angani mwaka mmoja uliopita, sasa hili ni tatizo
jengine linaloonekana kuitatiza Dunia... na pengine safari ya dunia ikawa ndio
mwisho kwani hata wataalam wa astronomia hawakuweza kuambua kitu,? Nchi nyingi
zilirudisha wataalam wake baada ya kuona kuwa zimebaki siku tatu kabda ya
kutokea kwa ajali hiyo kubwa na ya kwanza kutarajiwa viongozi wengi wa dini
walijua hicho ndicho kiama na hakiwezi kuzuilika, masaa machache dunia
ikagubikwa na giza nene na utafiti ukathibitisha kuwa uso wa esteroid hiyo
inaotarajiwa kupata ajari umeiinamia dunia na kuziba uso wa jua hivyo Dunia
yetu haitapata mchana tena japo ilithibitishwa kuwa ilikuwa hai ikiendelea
kujizungurusha na bado haikuwa imeguswa na kitu, miongoni mwa nchi zilizokuwa
na wataalam wakubwa wa sayansi ya anga ni pamoja na nchi ya Tanzania amapo
ilikuwa na wahitimu wa fani hiyo waliosoma vyuo mbalimbali Duniani zaidi ya
sabini, akiwemo mwanadada Mwantumu hamisi kiondo m bondei wa muheza Tanga
aliebahatika kusomeshwa na serikali kwenye chuo cha M.V. Lomonosov Moscow State
University, ambapo alihitimu vizuri sana na kuwa mmoja wa wanasayansi wa mambo
ya anga anaeaminika sana, tangu mwanzo wa ajali hii mwanadada huyu hakushiriki
kabisa ila sasa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alitia saini na jopo
la wana sayansi watatu wakitanzania wakishirikiana na warusi walipanda tena
angani huku mwanadada mwantumu akiongoza msafara huo, Dunia ilishakata tamaa
kwani watu waliutambua muda kwa kutazama saa tu maana Giza halikubadirika wala
kupambazuka, jopo hili lilifanikiwa kubadili nguvu ya mvutano na mhimili
ulioishika esteorid hiyo ulipokatika kuifanya esteorid hiyo kuelekea ilipo
sayari ya nne (mars) na Dunia kubaki kwenye usalama, Tukio hilo lilimpa heshima
kubwa mwantumu na Tanzania kwa ujumla hata Duniani kote kupatana kuipeperusha
bendera ya Tanzania kwa siku ishirini na moja mfurulizo. nakumbuka hatua ya
mwisho kabda ya kurejea Tanzania Mwantumu alialikwa Nchini america na baada ya
mwaliko akiwa njiani kurejea Tanzania ndege aliyokuwa akisafiria ilipata ajari
mbaya sana na kupelekea mwantumu na jopo lake lote kupoteza maisha, iliaminika
hivyo, hata waziri wa sayansi na tecnolojia alithibitisha kifo cha shujaa huyu
mwokozi wa Dunia na bendera zote Duniani kupepea nusu mlingoti, sasa mbona leo
hii namuona humu kwenye ndege hii ya kitecnolojia ya juu... ama ilikuwa ni
njama za wamarekani ili wammiliki wao? Mpeleke chumba namba tano kazi yake ipo
huko,,, profesor shivj solank aliekuwa jirani na mwantumu aliamrisha,
nililifahamu jina lake kwa haraka kwakua eneo aliloketi palikuwa na utambulisho
wa maandishi kumtambulisha yeye ninani, ila cha ajabu Eneo alilokuwa mwanadada
mwantumu lilikuwa na utambulisho wa siri (namba maalum iliyoandikwa ki 3D) Ghafla
nikasikia milio ya ndege za kivita kutokea nje. Kwa utaalam wangu nikatambua
kuwa ndege ninazozisikia ni aina ya Qaher-313 zilizotengenezwa iran zipatazo
kumi na saba na F-16 zipatazo saba. Tumevamiwa... Richard vipi unalalaaa.. kile
kipande cha mtu kilichoniteka kiliongea kwa kuchanganyikiwa punde mitambo
maalum yakisasa ya kudhibiti siraha za kiatomi ikawashwa na ile ndege ya
kitecnolojia ikaanza kuamka kwenda angani kitu kilichopelekea kile kipande cha
mtu kunikalisha chini na punde upepo mkali wenye baridi ya unyevu kushinda AC
ya kawaida ukaanza kutawala pale ndani... nikagundua sababu ya wenzangu wote
kuvaa ma jacket ya baridi...... +MTUNZI+ Mustapha J. Kiroboto (Moost Jay)