SHUJAA WA AFRICA BLOG

Sunday, August 19, 2018

RIWAYA YA NDEGE YA RAISI Ep 2


NDEGE YA RAISI:
NA MUSTAPHA J. KIROBOTO                                                                            (RIWAYA)
Sehemu ya pili
Ilipoishia.... muda huo ndege iliyobeba familia ya Raisi ilipita kasi karibu na pale na kushika anga,"Antony anafanya ninii..."catheline aliongea kwa kuchanganyikiwa...Aneth paisha helcopter hivyo hivyo tukawasaidie. Endelea......
Ni wazi kuwa hatutafanikiwa catheline.... ni ngumu kuiongoza ndege ikisha shika anga tusije kusababisha ajari kwa ndege zote tatu huko angani, Aneth alijibu huku akiirejesha helcopta chini, Aneth nimekwambia paisha helcopter...una mpango gani na maisha ya mheshimiwa?? Catheline aliongea kwa ukali... ila tatizo la anga na mawasiliano nimekujulisha... Amri...paisha helcopter nauifuate ndege ya mheshimiwa upesi nimuhamishe, Aneth akaamsha helcopter na kuidiriki anga... vipi aneth Ndege ya muheshimiwa imeelekea huku mbona unakwenda hukoo?! Si mimi ninaeipeleka catheline haitaki kwenda nitakako mimi:: Kitu gani tunatakiwa kufanya kwa wakati,huu? Mkuu wa usalama wa raisi alimuuliza Gerald rubani wa ndege ya raisi huku akizidi kuchanganyikiwa, sielewi ni spidi,kali mno tunayopelekwa nakili tangu nianze kuongoza ndege sijawahi tumia spidi hii, mungu wangu, vipi hali ya anga? Rada hazisomi... sina mawasiliano ya namna yeyote... mlango wa chumba cha dharula unagoma kufunguka tafadhari vunja vioo vya chumba toa parachut umpatie mheshimiwa, upesi sana mkuu wa usalama aliwahi alikoelekezwa na rubani ili kuhakikisha Raisi anaendelea kuwa salama, Vipi juu ya mwendo tunaokwenda kuna usalama kweli? Mheshimiwa Raisi alihoji huku akijiweka vizuri kwenye kiti, muda mwingi natafuta mawasiliano na Rubani lakini simptati...upesi nenda kaulize kama kuna tatizo tujue... Sawa mheshimiwa:: Tafadhari tujitahidi kuiongoza ndege irudi chini sielewi Dash board inachoniambia... Rubani wa ndege iliyobeba familia ya Raisi aliongea kwa kuchanganyikiwa... kuna niniii mbona ndege inakwenda tofauti.... kama kuna hitirafu tujue... mr andrew makema ndugu wa karibu wa Mheshimiwa Raisi msomi aliepewa cheo cha afisa usalama wa ikulu aliuliza, Ndege yetu haina mawasiliano mkuu... upesi telemsha ndege chini... aliamlisha... Tafadhari mkuu ameamlisha ndege ishuke chini... Taarifa ilifikishwa kwa Rubani wa ndege hiyo na muda huo ndege ikageuzwa kwaajili ya kushuka chini ikiwa kwenye kona kubwa ya dharula ndege ikapoteza mawasiliano na Muongoza ndege... punde taa zote za kwenye ndege zikazimika... jamani kitu gani kinaendeleo huko mbelee.... naamini ni hitirafu kubwa sana imetokea kwenye ndege yetu kwani inanigomea kuiongoza... Rubani alijibu huku jasho likimtoka... Tufanye nini marick?... upesi cheki power unit kama itaweza kuzalisha umeme .... Rubani alijibu huku akijaribu kuhangaika ili kuokoa tatizo hilo.... punde injini za ndege hiyo zikazima kwa awamu na ndege kuanza kurudi chini:::
 Nikauona mlango wa chumba changu umeongezwa upana kwa kukatwa ukuta kitaalam bila hata kuweka michanga, tii amri yangu kaa chini, kile kipande cha mtu kiliniamrisha tena... nikamtazama kwa umakini na kugundua kuwa hata ningempiga pigo kali kiasi gani lisinge mdhuru kutokana na ukubwa wa mwili wake kwakuwa watu wa namna hii hata siraha za kuwadhuru huwa ni maalum... taratibu nikapiga magoti mikono kichwani... punde akaingia mr allen mcLeod, afisa usalama wa america alienipokea pindi nilipotembelea nchini mwao kikazi, vipi ni ujio wa amani kwangu ama... bila ya kujibiwa swali langu nikapigwa pingu na kutolewa hadi kwenye ndege za kisasa zenye tecnolojia ya hali ya juu Zilizokuwa zimepaki nje ya nyumba yangu.. sifa ya ndege hizi niliwahi kuipata nilipokuwa Saratov Rashia ni ndege zenye uwezo wa juu sana ki ulinzi, na zaidi zina vifaa maalum vyakuweza kuzima mitambo ya mawasiliano kwa upana wowote wa eneo unalotaka kulivamia, ndani ya chumba maalum kwenye ndege ile nikawakuta mwanadada mwantumu hamisi kiondo akiendelea kuongoza mitambo, macho yalinitoka nikiwa siamini ninachokiona::
Takribani miezi tisa iliyopita Dunia iliwahi kupatwa hofu kubwa ya kuteketea kutokana na wana sayansi wa kimarekani kugundua kuisha kwa mhimili mkuu ulioishika moja ya asteoridi (Gimba kubwa au Jiwe lililo mfano wa sayari nyengine) ambapo ulibakia nyuzi chache mhimili huu kukatika na tukio hilo kupelekea asteoridi hiyo ya ukubwa wa kuizidi Dunia kwa zaidi ya takribani kilometa tilioni mia saba kila upande ( mraba) kuiangukia Dunia na pengine huo ndio ungekuwa mwisho wa dunia kwani kwa vipimo vya wataalam ilionekana Dunia ingeathirika kwa zaidi ya asilimia mia moja na ishirini na nne ya eneo lake, Nchi nyingi kubwa Duniani zilituma wataalam wake ili kupambana na tatizo hilo kwa ajili ya kuiokoa Dunia lakini hali ilikuwa tete na mhimili huo ulioishika esteorid ulizidi kuathilika kiasi cha kubakisha masaa mia moja stini na nne (164) sawa na siku saba (7) kabda ya kukatika na kuiachia esteorid hiyo iliyokuwa imeelekea kuiangukia sayari ya earth. (Dunia) Jopo la wanasayansi lililokuwa juu angani lilianza kugawanyika kwa hofu, wengi walirejea ili kufa pamoja na familia zao ila wengine walijitahidi kukaza madini ya namna mbali mbali kwenye mhimili huo lakini kiukweli hayakuweza kuleta mafanikio, Wanasayansi wa Urusi walirudi nchini kwao kwa dharula nakukutana na waziri mwenye dhamana ya mambo hayo... urusi ilipata jina kubwa sana mwaka mmoja nyuma baada ya wahitimu wa sayansi ya anga kufanikiwa kutengeneza kifaa maalum cha kuikinga Dunia na milipuko mikali ya volcano iliyotokea huko angani mwaka mmoja uliopita, sasa hili ni tatizo jengine linaloonekana kuitatiza Dunia... na pengine safari ya dunia ikawa ndio mwisho kwani hata wataalam wa astronomia hawakuweza kuambua kitu,? Nchi nyingi zilirudisha wataalam wake baada ya kuona kuwa zimebaki siku tatu kabda ya kutokea kwa ajali hiyo kubwa na ya kwanza kutarajiwa viongozi wengi wa dini walijua hicho ndicho kiama na hakiwezi kuzuilika, masaa machache dunia ikagubikwa na giza nene na utafiti ukathibitisha kuwa uso wa esteroid hiyo inaotarajiwa kupata ajari umeiinamia dunia na kuziba uso wa jua hivyo Dunia yetu haitapata mchana tena japo ilithibitishwa kuwa ilikuwa hai ikiendelea kujizungurusha na bado haikuwa imeguswa na kitu, miongoni mwa nchi zilizokuwa na wataalam wakubwa wa sayansi ya anga ni pamoja na nchi ya Tanzania amapo ilikuwa na wahitimu wa fani hiyo waliosoma vyuo mbalimbali Duniani zaidi ya sabini, akiwemo mwanadada Mwantumu hamisi kiondo m bondei wa muheza Tanga aliebahatika kusomeshwa na serikali kwenye chuo cha M.V. Lomonosov Moscow State University, ambapo alihitimu vizuri sana na kuwa mmoja wa wanasayansi wa mambo ya anga anaeaminika sana, tangu mwanzo wa ajali hii mwanadada huyu hakushiriki kabisa ila sasa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alitia saini na jopo la wana sayansi watatu wakitanzania wakishirikiana na warusi walipanda tena angani huku mwanadada mwantumu akiongoza msafara huo, Dunia ilishakata tamaa kwani watu waliutambua muda kwa kutazama saa tu maana Giza halikubadirika wala kupambazuka, jopo hili lilifanikiwa kubadili nguvu ya mvutano na mhimili ulioishika esteorid hiyo ulipokatika kuifanya esteorid hiyo kuelekea ilipo sayari ya nne (mars) na Dunia kubaki kwenye usalama, Tukio hilo lilimpa heshima kubwa mwantumu na Tanzania kwa ujumla hata Duniani kote kupatana kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa siku ishirini na moja mfurulizo. nakumbuka hatua ya mwisho kabda ya kurejea Tanzania Mwantumu alialikwa Nchini america na baada ya mwaliko akiwa njiani kurejea Tanzania ndege aliyokuwa akisafiria ilipata ajari mbaya sana na kupelekea mwantumu na jopo lake lote kupoteza maisha, iliaminika hivyo, hata waziri wa sayansi na tecnolojia alithibitisha kifo cha shujaa huyu mwokozi wa Dunia na bendera zote Duniani kupepea nusu mlingoti, sasa mbona leo hii namuona humu kwenye ndege hii ya kitecnolojia ya juu... ama ilikuwa ni njama za wamarekani ili wammiliki wao? Mpeleke chumba namba tano kazi yake ipo huko,,, profesor shivj solank aliekuwa jirani na mwantumu aliamrisha, nililifahamu jina lake kwa haraka kwakua eneo aliloketi palikuwa na utambulisho wa maandishi kumtambulisha yeye ninani, ila cha ajabu Eneo alilokuwa mwanadada mwantumu lilikuwa na utambulisho wa siri (namba maalum iliyoandikwa ki 3D) Ghafla nikasikia milio ya ndege za kivita kutokea nje. Kwa utaalam wangu nikatambua kuwa ndege ninazozisikia ni aina ya Qaher-313 zilizotengenezwa iran zipatazo kumi na saba na F-16 zipatazo saba. Tumevamiwa... Richard vipi unalalaaa.. kile kipande cha mtu kilichoniteka kiliongea kwa kuchanganyikiwa punde mitambo maalum yakisasa ya kudhibiti siraha za kiatomi ikawashwa na ile ndege ya kitecnolojia ikaanza kuamka kwenda angani kitu kilichopelekea kile kipande cha mtu kunikalisha chini na punde upepo mkali wenye baridi ya unyevu kushinda AC ya kawaida ukaanza kutawala pale ndani... nikagundua sababu ya wenzangu wote kuvaa ma jacket ya baridi...... +MTUNZI+ Mustapha J. Kiroboto (Moost Jay)

No comments:

Post a Comment